Welcome!

I am John Doe Web Designer Photography

View Work Hire Me!

About Me

Web Design
Branding
Development
Who am i

John Doe.

Professional Web Designer

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat condimentum velit class aptent taciti sociosqu ad litora.

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat condimentum velit class aptent taciti sociosqu ad litora torquent metus metus ullamcorper vel tincidunt sed class aptent taciti sociosqu ad litora .

Services

Web Design

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat

Development

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat

Branding

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat

Marketing

Nulla metus metus ullamcorper vel tincidunt sed euismod nibh Quisque volutpat

Our Blog

Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Makamba: Operesheni sitisha viroba iko pale pale

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),January Makamba (kushoto) akiwaonyesha wanahabari simu yake ambayo ilikuwa na habari iliyochapishwa na Mwananchi kuhusu katazo la pombe za viroba ifikapo Januari Mosi mwaka huu. Kulia ni  Katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa Faustine Kamuzora.Picha na Bakari Kiango.

By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

NEC to study Chadema claims over 'blank' BVR cards

The National Electoral Commission yesterday promised to study claims by Chama cha Demokrasia na  Maendeleo (Chadema) that over two million blank BVR cards meant to tilt results of the October General Election are in illegal circulation.
The NEC chairman (retired), Judge Damian Lubuva
The NEC chairman (retired) Judge Damian Lubuva told the Guardian yesterday in a telephone interview when reacting to allegations by Chadema   that the Commission in collaboration with Chama Cha Mapinduzi  (CCM) were all out  to temper with October election results.
Lubava said the Commission could not work on rumours and that it s waiting for Chadema to submit official complaints.
 “If the party has details on the matter it should bring them to us and then we will work on them immediately instead of going to the media,” Lubuva said. 
“The Commission is fulfilling its obligations without any pressure from any political party or government. I have no enough details on this matter unless I receive official complaints from Chadema and we will work on them and announce our findings,” he added.
He however assured the public that there will be no vote rigging in the coming elections because NEC is fulfilling its obligations by abiding by the laws.
Speaking to the media yesterday in Dar es Salaam chairperson of Chadema Women Wing Halima Mdee accused NEC of being used by CCM to tamper  with votes counting.
She said that over two million voters’ cards have been produced despite the fact that the process has been concluded in order to steal votes in the coming General Election.
According to her an informant from NEC had communicated the information to Chadema after uncovering the plot by CCM and NEC to rig the elections.
She said CCM had organised particular people who move from house to house bribing people so that they can provide their personal details available in their voter cards so that they can reproduce them.  
 “I call upon people not to sell their votes by any means…I urge you to ignore such people who come to”, said Mdee.
  She also called upon NEC to be serious with the verification process because up to now there was a likelihood that many people will not verify their information.
“Voter verification in Dar es Salaam is also a problem which NEC to solve it once and for all…we want people to verify their names at the centres where they registered and not at wards as the Commission had announced so as to enable every one to verify the information,” she added.
For his part, Saed Kubenea, Ubungo constituency aspirant on Chadema ticket said that the party had in hand 150 such  voters cards. 
He said NEC has been fabricating election results for several years but in this year it will not succeed because the people themselves are tired.
“You know people’s awareness had increased as they were now tired of hard times and they are now ready   for  change in the coming General Election,” he said.
Over the weekend the Guardian on Sunday had reliably established that Biometric Voter Registration (BVR) System has been put into serious question with only two months ahead of the October General Election  as it failed to detect voters who registered more than once, contrary to reassurance by the National Electoral Commission (NEC). 
It established that some individuals may have registered themselves more than once under BVR devoid of detection by the reputed high security system.  
At issue is the unraveling of two BVR cards belonging to a voter identified as Samwel S Choggo, courtesy of an individual who preferred anonymity but had an access to the system’s underworld. 
According to the details in the cards, Choggo who was born on January 1, 1991 registered himself at Dovya Street, Bunju Ward in Dar es Salaam Region where he was issued voter’s card No.T-1000-0906-706-4. 
But a person of the same name born on the same date, with a rather twisted snapshot pose and in a different shirt holds voter’s card No.T-1003-5915-554-3 registered at Miswe Chini Street, Mbwawa Ward.
Contacted, NEC’s Director of Election Kailima Kombwey said voters will now use the old voting system using BVR cards, and that there wouldn’t be any computer or BVR machines to trace their verification.
SOURCE: THE GUARDIAN

Govt seeks media support for sexual, reproductive health

The mass media must be the core partner in advocating rights of sexual and reproductive health if the fight against children’s and maternal related deaths in Tanzania should be intensified.
 
This was said recently by the National Coordinator for Safe Motherhood, Dr KohelethWinani, at the launch of the Media Network for Sexual and Reproductive Health Rights (Tamenet-SRHR).  
 
He emphasized: “The war against infant and maternal death must involve many stakeholders; so the media must use their profession and convey to communities correct information about safe sex and reproductive health.” 
 
He said Tanzania can contain most maternal related deaths if the right information on best ways to handle the problem is disseminated.
Dr Winani was representing the permanent secretary in Ministry of Health and Social Welfare, Dr Donald Mmbando, at the occasion.
 
For his part, the network’s acting chairperson, Hussein Siyovelwa, said media coverage of sexual and reproductive health rights was crucial in achieving national development goals. Yet journalists covering them often face significant challenges, he lamented.
 
He said 25 journalists made the decision to form the network in 2013. This was after undergoing intensive training provided by an organization known as Tanzania Men as Equal Partners (TMEP) that works under a Swedish organization called RFSU. 
 
He said: “After the launch of the network we hoped to reduce challenges in reporting on the subject. We also hoped that we would be able to speak and educate the public on issues concerning sexual reproductive health rights.”
 
Tanzania has achieved the WHO target of reducing the child mortality rate to 54 in every 1,000 live births. But, despite the number of deaths plummeting from 520 to 432 in every 100,000 live births, the target is to reach 193 deaths in every 100,000 live births
SOURCE: THE GUARDIAN

Business community planning 'dialogue' for presidential candidates

The Tanzania business community plans to conduct a dialogue that will bring together all the presidential candidates in the forth coming General Election , the group chairman Johnson Minja said here last Saturday.
 
Johnson Minja
Minja who led the group in protest against the government’s recently introduced Electronic Fiscal Devices (EFDs) several months ago, however was quick to affirm that they werenot behind any presidential aspirants.

“All we want is for the candidates to candidly explain what they can do to improve the business environment and to change lives of ordinary Tanzanians” he said, adding that the date for the dialogue will announced later.
 
Speaking during a one- day annual meeting of the business community in Dodoma last Thursday evening, Minja warned that members of the group shall not vote for any candidate who will fail to attend the dialogue.
 
He said any presidential aspirant who fails to participate in the dialogue shall have approved to them that he or she does not need their votes following failure to listen to them.
 
Minja who enjoys support of fellow business members clarified that the dialogue also will be attended by representatives from other groups like farmers, pastoralist and workers.
 
Unlike other dialogues, he said political parties representatives shall not be allowed to wear part colours or anything that easily identify them with any party as business members shall wear dark suits.
 
“We shall attend the dialogue without any formed opinion but shall come out of it with a decision on who to support, depending on the debate” he stated but warned those engaging in politics to stop as it is not possible to do politics and business at the same time.
 
Officiating the launch of the annual meeting on behalf of the Regional Commissioner, Dodoma District Commissioner, Dr Jasmin Tiisekwa urged the business community to shy away from united partisan politics.
 
She said the group should not be used by politician in effort to support one candidate for the state house race, saying such a move can trigger violence in the country.
 
“It would be surprising to see your group getting involved in dirty political issues instead of pushing working hard to improve your welfare” she noted.
 
The DC said just like any other Tanzanian, they have the constitutional right to vote for any candidate they think will work for their benefits and other people without interfering with the existing peace.
 
She openly reminded the business people that peace is the most fundamental factor for development of any nation and without it they cannot operate businesses.
SOURCE: THE GUARDIAN

Baadhi ya viongozi na waumini wa dini ya kikristo wameamua kuanza kufanya maombi maalum

Baadhi ya viongozi na waumini wa dini ya kikristo wameamua kuanza kufanya maombi maalum kwa wiki moja kuanzia kesho kumuomba mwenyezi mungu aliepushe taifa na ajali ambazo katika kipindi cha mwezi january mpaka mwezi huu watu 866 wamekufa huku zaidi ya 2400 wakijeruhiwa. 
Mwenyekiti wa maombi hayo mch. Dr.Getrude Rwakatare amewaambia waandishi wa habari kuwa kupitia maombi hayo wanatumai wimbi la ajali hizo litapungua

Akinamama wajawazito waonywa kutotumia dawa za kuongeza uchungu wakati wa kujifungua

Akina mama wajawazito kote nchini wameshauriwa kutotumia dawa za kienyeji  kwaajili ya kuongeza nguvu za uchungu wakati wa kujifungua hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha  yao na kupelekea vifo kwa akinamama wengi nchini.
Akiongea katika hospital ya Kagondo  mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Thomas Ruta amewataka akinamama wajawazito kufika katika vituo vya afya mara kwa mara ili waweze kuchunguzwa afya zao  na kuongeza kuwa hospital ya kagondo  imekuwa na umuhimu mkubwa katika mkoa huo na taifa kwa ujumla kwani kutokana huduma bora zinazo tolewa katika hospital hiyo  kumesaidia kuipunguzia mzigo hospitali ya rufaa ya mkoa wa kagera ambayo ilikuwa ikipokea mamia ya wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali kila kukicha.
 
Kwa upande wake Rais  na mkurugenzi  mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali  la Jhpigo kutoka nchini marekani  ambalo limekuwa likijishughuli katika kutoa huduma za afya ya uzazi kwa akina mama na watoto walio chini ya miaka mitano  Leslie Mancuso ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na huduma zinazotolewa kwa akinamama na watoto katika hospital ya hospital hiyo na kwamba shirika hilo sasa  lita jikita zaidi katikakuongeza vifaa tiba katika hospital hiyo  ikiwemo huduma ya usafiri kwa wagonjwa kwaajili ya kunusuru vifo kwa akinamama wajawazito na watoto. 
 
Nae muunguzi afisa muunguzi wa wodi ya akinamama wajawazito PASCHAZIA HENRY amesema pamoja na huduma zinazotolewa katika hospitali lakini bado kuna changamoto nyingi  ikiwemo upungufu wa wahudumu kwani kunawakati wanapokea wagonjwa wengi kupita kiasi huku katibu wa hospital hiyo JOSHUA JOSEPH akiwataka akina mama wajawazito kuepukana na imani potofu za kutumia dawa za kuongeza nguvu ya uchungu wakati wakujifungua kwani zimekuwa zipelekea vifo kwa akinamama wengi nchini badala yake wafike katika hospital pamoja na vituo mbali vya afya ili waze  kupata ushauri nasaa juu ya afya  ya uzazi kwa mama na watoto

Wafanyabiashara Songea wasaidia waliokumbwa na maafa.

Wafanyabiashara wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma   kwa kushirikiana na serikali  wamezisaidia  chakula, vifaa  vya ujenzi pamoja na fedha    kaya  kumi na sita zilizokuwa zikilala nje  baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo   katika  kata ya matarawe    mkoani humo.
Mwenyekiti wa jumiya ya wafanyabiashara mkoa wa Ruvuma Bw. Tito Mbilinyi amemkabidhi  katibu  tawala wa wilaya ya songea Bw.Ally Juma vifaa hivyo vikiwa na thamani ya   shilingi  1992,000 ikiwa  pamoja na pesa huku serikali ikiwa imechangia s hilingi  885,000 na kufanya jumla ya pesa zote kuwa milioni mbili elfu themanini na sabini na tano ili awakabidhi wahanga wa  maafa yaliyotokea aprili tano na kuziacha  kaya kumi na sita zikilala  nje.
 
Katibu tawala huyo ameshukuru kwa mchango huo wa wafanyabiashara.
 
Nao wananchi waliokumbwa na maafa hayo matarawe songea  aprili tano siku  ya pasaka wameshukuru kwa msada huo kwa kuwa walikuwa wanalalaa nje.

Sitta: Huu ni mtaji wangu wa urais

Dar es salaam. Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasubiri kukamilika kwa utaratibu wa CCM wa kugombea urais ili aingie rasmi kwenye mbio hizo kwa kuwa anaridhika na mambo matatu ambayo anasema yanamfanya ashawishike kugombea nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini.
Sitta, mwanasiasa mkongwe na Spika wa Bunge la Tisa, ni mmoja kati ya makada wa chama hicho tawala wanaotarajiwa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais kumrithi Jakaya Kikwete, ambaye anamaliza vipindi vyake viwili vya urais Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Sitta alisema zaidi ya mambo hayo matatu, anaamini ana ushawishi mkubwa na Watanzania wengi wanamwamini katika utendaji kazi wake.
“Nina mengi nimefanya kutokana na historia yangu ya kiutendaji na ndiyo nitakayoitumia kama mtaji utakaonibeba kwenye harakati hizi,” alisema.
Sitta, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, alitaja mambo hayo matatu ambayo ni mtaji wake kuwa ni uendeshaji wake wa chombo hicho cha kuandika Katiba, uendeshaji wake wa Bunge na uzoefu wake wa muda mrefu kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kushika.

“Niliendesha Bunge la Katiba kwa mafanikio na hata kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa,” alisema Sitta.
“Watanzania wataangalia wenyewe historia yangu kwani mimi ndiye mwenyekiti niliyefanikisha kutimiza ndoto za Watanzania kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalumu la Katiba, haikuwa rahisi katika tukio hilo,” alisema.
Hata hivyo, Bunge la Katiba halikuisha kwa maridhiano baada ya wajumbe kutoka vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kususia vikao kwa madai kuwa chombo hicho kiliweka pembeni Rasimu ya Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi.
Juhudi za Sitta kuwarejesha vikaoni ziligonga mwamba, lakini mchakato ukaendelea hadi Katiba Inayopendekezwa ilipopatikana.
Sitta alisema mtaji wake mwingine katika mbio za urais ni na kuimarisha demokrasia ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
“Mimi ndiye niliyebadilisha Bunge baada ya kubadilisha kanuni za Bunge mwaka 2007, ambazo zilitoa uhuru, haki na usawa kwa wabunge wote bila kujali wapinzani,” alijigamba“Bunge langu ndilo liliibua umaarufu wa wapinzani na ndipo wakaibuka akina Zitto Kabwe na Dk Wilbroad Slaa kwani walipata nafasi ya kuibua hoja na kuhoji udhaifu wowote wa Serikali.”
Sitta alisema haikuwa rahisi kufanya mabadiliko hayo kwani baadhi ya wanachama wenzake walipingana na jambo hilo, lakini alilisimamia kama Spika na kulipeleka bungeni.
“Nilipingwa sana lakini nikasema hapana, kuna Tunu za Taifa zilizokuwa zimeharibiwa na lazima tuzirejeshe na matokeo yake kwa sasa yameanza kuonekana,” alisema.
“Hata katibu mkuu wetu wa CCM, Abdurahman Kinana ambaye anakosoa Serikali na kuagiza uwajibikaji, siyo kuwaachia wapinzani tu, anayaona na anasema kwa kuwa wanaofanya hayo yanayoonekana ni watu wetu ndani ya CCM,” alisema Sitta.
Alisema jambo la tatu ni uzoefu wake katika utawala kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa.
“Nimefanya kazi na marais wa awamu zote, wananikubali kwa kuwa mimi ni mchapakazi. Wasingekuwa wananichukua kama si mchapa kazi,” alisema Sitta ambaye ana umri wa miaka 73.
Lakini, mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema kwa sasa Taifa lipo kwenye kipindi kigumu.
“Katika kipindi hiki, lazima Watanzania wachuje na waangalie ni kiongozi gani atakayewafaa katika uongozi ujao na si kukurupuka na kudanganywa,” alisema.
Sitta pia aligusia mgogoro uliopo baina ya Serikali na viongozi wa dini kuhusu Katiba Inayopendekezwa, akisema ni makosa kwa viongozi hao wa kiroho kuingilia masuala la kisiasa.
Alisema si kila kilichohitajika kuingia kwenye Katiba, kingepita sasa.
“Mazuri na mambo yote ya msingi yameingizwa kwenye Katiba hiyo na siyo rahisi kulazimisha maoni ya kila mtu yaingie, wasubiri labda kwa kipindi kijacho yataingia,” alisema.
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo wameagiza waumini wao waikatae Katiba Inayopendekezwa wakidai Serikali iliahidi kuingiza suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba ili Waislamu wakubali kuipitisha, jambo ambalo linachukuliwa kuwa ni kuingilia masuala ya kisiasa.

Serikali imekubali kuviondoa vijiji 21 vilivyo chukuliwa kuwa sehemu ya Hifadhi yaTaifa ya Ruaha wilayani N barali

Serikali imekubali kuviondoa vijiji 21 vilivyo chukuliwa kuwa sehemu ya Hifadhi yaTaifa ya Ruaha wilayani N barali , ili kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ambao umedumu kwa miaka saba.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa LAZARO NYALANDU amesema hayo katika mkutano wa hadhara katika eneo la U baruku, wilayani Mbarali ambao kabla wananchi wamemueleza kwa kirefu kiini cha mgogoro huo na kuapa hawataruhusu hata kitongozi kimoja kuchukuliwa tena na hifadhi kwa madai kuwa maeneo yao yanachukuliwa bila kufuata sheria

Chama cha walimu CWT cha mpongeza Rais JAKAYA KIKWETE SOMA HAPA ZAIDI:

Chama cha Walimu Tanzania CWT kimeridhia hatua ya kuundwa kwa chombo kimoja cha kusimamia ajira za walimu na kusema Rais JAKAYA KIKWETE atakumbukwa kwa uamuzi wa serikali yake kuunda chombo hicho na kubadili muundo wa utumishi wa walimu.
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CWT Bwana EZEKIEL OLOUCHI wakati wa kongamano la wadau la wadau wa elimu kuzungumzia maslahi ya walimu.

BAADA YA KUSHAMBULIA KENYA, WATU 10 WAKAMATWA KWA UGAIDI TANZANIA

Morogoro.
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) milipuko hatari aina ya 'water explosive gel' iliyokamatwa jana usiku kutoka kwa watuhumiwa 10 waliokuwa wamehifadhiwa ndani ya msikiti wa Sunni uliopo tarafa ya Kidatu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Katika tukio hilo, mmoja anayesadikiwa kuhusiana na watu hao waliokamatwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa panga askari polisi aliyekuwa akipambana naye.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.Kamanda Paul alimtaja mtu aliyefariki kuwa ni Hamad Makwendo ambaye umri wake haujafahamika ambaye ni mkazi Manyasini Ruaha wilayani Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.

Kamanda akionesha vilipuzi
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Paul alisema: “Polisi walipata taarifa kuwa watu hao walitumia usafiri wa bajaji mbili kwenda kusikojulikana na wakati wakiendelea na zoezi la kufuatilia ndipo walikutana na bajaji moja ikiwa na abiria mmoja ambaye ni Mkwendo na kuisimamisha.”
Alisema kuwa bajaji hiyo iliposimama marehemu huyo aliruka na kuanza kukimbia ndipo askari mwenye namba F .3323 Koplo Nasoro alianza kumkimbiza na alipomkaribia mtuhumiwa huyo alichomoa jambia alilokuwa nalo na kumkata askari huyo eneo la shingoni.
Askari mwingine mwenye namba E.9245 Koplo Chomola ambaye alikuwa nyuma alifanikiwa kumpiga risasi ya mguu mtuhumiwa huyo, ambapo alipoanguka chini wananchi wa eneo hilo tayari walifika katika eneo hilo na kuanza kumshambulia marehemu huyo kisha kumchoma moto kwa hasira.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu wengine ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka.”
Alisema polisi walendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni.

Baadhi ya vifaa vilivyokamatwa msikitini na polisi ambapo watu 10 wanashikiliwa na jeshi hilo mjini Morogoro.
Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokutwa katika mabegi yaliyokuwa ndani ya msikiti huo ni pamoja na milipuko 30, bendera nyeusi yenye maandishi ya Kiarabu yakisomeka ‘Mungu Mmoja’, majambia, bisibisi, vinyago vya kuziba uso (masks), nguo za jeshi, misumeno ya chuma na spana.

Gwajima: Kikwete wakemee polisi wanaoniandama

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo vya dola vinavyomfuatafuata vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa kufanya hivyo itakuwa wazi kwamba yeye ndiye anawatuma.
Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo jana, Gwajima alisema amekuwa akifuatwafuatwa na vyombo vya Serikali utadhani yeye si raia wakati ni Mtanzania halisi.
“Rais Kikwete tafadhali namuomba awakemee watu hawa... asipowakemea, basi kanisa langu litajua kwamba yeye ndiye anayewatuma,” alisema Gwajima huku akishangiliwa na waumini waliokuwa wakimsikiliza.
Huku wakinyeshewa na mvua, waumini hao walikuwa wakimsikiliza Askofu Gwajima, siku tatu baada ya kiongozi huyo kuhojiwa kwa mara ya pili na polisi na kutakiwa awasilishe mambo 10 yanayohusiana na usajili wa kanisa, uongozi na mali zake.
Uraia wake
“Mimi ni Mtanzania halisi acheni nifanye kazi ya Mungu, kama mnadhani mimi si Mtanzania, basi mmepotoka kwani kwa hilo mtashindwa,” alisema.
Alisema makundi ya jamii yamekuwa yakitoa kauli mbalimbali lakini hayabughudhiwi anavyofanyiwa.
“Madaktari, wanasiasa, wafanyabiashara wamekuwa wakitoa misimamo yao lakini hawabughudhiwi iweje Gwajima tu? Nitaendelea kuwapa vidonge vyenu kila mtakapopotoka, nafanya kazi ya bwana,” alisema.
Kuhusu utajiri wake
Gwajima alisema amekuwa akishangazwa na vyombo vya Serikali vinavyohoji utajiri alionao bila kujua anaongoza idadi gani ya waumini. Alisema anaongoza kanisa lenye waumini zaidi ya 70,000 ambao ni kama watoto wake na kwamba yeye ni baba yao wa kiroho.
“Waumini hawa mimi ni baba yao wa kiroho, nikiwaomba kila mmoja anipe Sh1,000 tu nitakuwa na Sh70 milioni, halafu mnahoji utajiri ninaupata wapi?” alisema na kisha kuwauliza waumini hao... “Hivi baba yenu nikiwaomba kila mmoja anipe Sh1,000 mtanipa au mtaninyima?”
Alijibiwa, “Tutakupaaaa!” Baada ya majibu hayo waumini hao walianza kupeleka fedha katika jukwaa kuu huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu.Waumini hao, wengi wao wakiwa wameshikilia noti za Sh10,000 na Sh5,000 walianza kusonga mbele na kutumbukiza kwenye maboksi.
Mchango huo ulichukua dakika 25 kuanzia saa 6.30 hadi saa 6.55 mchana na ulisimama pale Askofu Gwajima kuwaambia... “Basi basi naomba muache kuleta fedha, zinatosha, kaeni msikilize mahubiri, tukiendelea kupokea fedha hapa tutakesha. Watu wa idara ya fedha kusanyeni maboksi yenye fedha na pelekeni kunakohusika, hizi ni fedha za kanisa ambazo zitatumika katika mambo mbalimbali ikiwamo kununua mafuta ya kuendesha jenereta la kuzalisha umeme.”
Gwajima alisema kutokana na idadi ya waumini wake kama kila mmoja atampa Sh10,000 basi atakuwa na Sh700 milioni.
“Wakinipa Sh100,000 kila mmoja ina maana nitakuwa na Sh7 bilioni, nawashangaa wanaohoji kuwa huu ni utajiri, watu hawalali usingizi wanajiuliza Gwajima anapata wapi utajiri huu, nawaambia mimi siyo tajiri hizi ni fedha za kanisa,” alisema.
Idadi ya waumini
Askofu huyo alisema mbali na utajiri, watu wanahoji anapata wapi waumini wengi namna hiyo.
“Shida si kumkashifu Askofu Pengo, bali sasa wanahoji waumini wengi wanafuata nini hapa,” alisema na kuongeza,” nao wakija kunisikiliza watafahamu nini mnachokifuata kwani nao watabaki hapahapa hawatatoka.”
Alisema baada ya kuandamwa na vyombo vya Serikali, maaskofu walitaka kutoa tamko lakini aliwakataza kwa sababu aliona anafanyiwa hivyo kwa sababu binafsi. Alisema katika kipindi ambacho amekuwa akiandamwa na polisi, waumini wameongezeka kanisani kwake.
“Walokole wakiwa katika tabu, ndiyo kwanza wanashikamana, ukitaka kuwasambaratisha wape neema utafanikiwa. Wakipata nyumba nzuri, gari zuri, kazi nzuri na safari katika nchi mbalimbali wanaacha kuja kanisani lakini wakiwa katika matatizo wanashikamana, hamuwezi kuwasambaratisha,” alisema.
Ilivyokuwa awali
Gwajima amehojiwa mara mbili na polisi kutokana na matamshi yake ya kashfa dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, lakini mara ya pili mwelekeo wa mahojiano ulibadilika ukalenga zaidi kanisa na mali zake.
Mara ya kwanza kuhojiwa ilikuwa Machi 27, siku ambayo alizimia na kupelekwa katika Hospitali ya TMJ alikolazwa kwa siku nne huku taarifa zikieleza kuwa alishtushwa baada kuhojiwa mambo yake binafsi badala ya tuhuma alizoitiwa polisi.Baada ya kutoka Polisi, Gwajima amekuwa akitembea kwa kutumia kiti cha magurudumu mawili hadi Aprili 6, Siku ya Pasaka baada ya kuombewa na wachungaji kutoka Japan.
Alhamisi iliyopita, alihojiwa kwa mara ya pili na kutakiwa kurudi tena Polisi Aprili 16 akiwa na mambo 10 yakiwamo hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la Wadhamini, idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia, nyaraka za helikopta ya kanisa, muundo wa uongozi wa kanisa, waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za kanisa na nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari.

Mamia ya wananchi wa kilosa na kilombero washiriki katika mazishi ya pamoja kwa abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Nganga.

Mamia ya wakazi wa wilaya za kilosa na kilombero  wamejitokeza    katika mazisha  ya pamoja ya  watu kumi na tano kati ya kumi na tisa waliofariki katika ajali ya basi ya nganga ambalo liligongana na fuso  kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi  na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa mkoani Morogoro.
Wakizungumza kwa niaba ya serikali mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu waliofariki kwenye  ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari amkoani  wa Morogoro ili kudhibiti ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na vilemalema  vya maisha   ambapo mkuu wa wilaya ya kilombero Bw Lephy Gembe amewataka  wananchi  kuwa na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.
Kwa upande wake Diwani  wa kata ya ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi wa wilaya hizo huku ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo siwakusahaulika kwani umewastua sana ambapo naye  muinjilisti wa kanisa la kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na madereva wabovu.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa ibrahim haruna lipumba

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa ibrahim haruna lipumba na wanachama wengine 30 wafuasi wa chama hicho leo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam wakishtakiwa kwa kosa la kuandamana bila kufuata utaratibu.
Baadhi ya watu waliohudhuria shauri hilo ni pamoja na makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Jeshi la polisi mkoani katavi linawashikilia watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujangil

Jeshi la polisi mkoani katavi linawashikilia watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujangili, baada ya kuwakamata na vipande vinane vya meno ya tembo vyenye uzito wa zaidi ya kilo nane,na vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49na laki tano ambavyo vinaonesha kuwa tembo wawili wameuawa ili kupatikana kwa nyara hizo za serikali.

Kiongozi wa chama cha ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT)

Kiongozi wa chama cha ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT) wazalendo bwana Zitto Kabwe amesema mfumo wa kiuchumi unaowabeba na kuwanufaisha watu wachache ndiyo sababu ya kuendelea kudidimia kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuongezeka kwa umaskini wa kipato licha ya uchumi wa nchi kutajwa kukua kwa asilimia saba kwa mwaka

Wema:azomewa licha ya Kujieleza

Muigizaji maarafu wa filamu nchini Tanzania,Wema Sepetu alizomewa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kuweka picha ya mlimbwende Hamisa Obetto akiwa mjamzito na kuandika maneno ya mshangao
”Jamani my mdogo umezaa.!wewe ni mwanamke sasa”.
Ujumbe huo ulizusha tafrani kwa baadhi ya watu na kumjibu Wema kwa maneno makali yenye kebehi ya
kwa nini yeye hazai anakaa kushabikia watoto wa wenzie tu.
Gumzo hilo lilifwata mkondo tofauti pale ambapo mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum
akitarajia kupata mtoto na bi.Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani wake mkubwa Wema.
Wema Sepetu aliweza kujibu tuhuma hizo kwa kusema yeye si mpanga wa yote,''ningekuwa na uwezo wa kuzaa angezaa siku nyingi ila ni Mungu ndiye anapanga'',
Alisema kuwa ''nimekuwa nikihangaika kupata mtoto usiku na mchana''
aliongezea kusema kuwa si rahisi kwa yeye kuwaambia kila kitu,kwani yeye pia ni binadamu na kuwa
''anaumia sana na maneno makali watu wanayoandika au kusema kumhusu''.
Ujumbe wa simanzi kutoka kwa muigizaji huyo ulirudiwa na baadhi ya waigizaji kama Iren Uwoya na mashabiki wengine
ukionya tabia ya watu kutoa matusi makali kwa Wema bila kuangalia upande wa pili,maana siku hizi kuna team kwenye mtandao pia zikijiita team Wema na Team Zari

Baada ya kusakamwa kwa muda mrefu kuhusu suala la kutopata mtoto hatimaye Wema Sepetu amefunguka hivi:
""Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana... But sina... Na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu.... Au mngependa niwe nawaambia jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe... Is dat wat u want...? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze... Au mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto.
"kumbukeni na mimi pia ni binaadam... Nina moyo kama nyie...Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa...Mnaona nafurahia sio....Hivi mna nini jamani...Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu...Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashifu na kunitolea maneno mazito namna hio... Kisa mtoto... Mnadhani naipenda hii hali... Hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho.... So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die... Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua... Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu... I want dat with all my life but I cant.... Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kaniandikia... But just dont rub it in... It hurts... And im jus a human being like each and everyone of u."

Bei za umeme kushuka zaidi Julai

Dar es Salaam. Kuanzia Julai mwaka huu Watanzania wataanza kupata umeme wa uhakika na usiyo kuwa na gharama baada ya kuanza kazi kwa mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi, utakaoingiza kwenye gridi ya Taifa megawati 150.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Injinia Felchesmi Mramba wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kinyerezi na vituo vya kupokea na kusambaza umeme vya Gongolamboto, Kipawa na Ilala City Center, vyote vya Dar es Salaam.
Alisema kuna uwezekano mkubwa wa bei za umeme kushuka, iwapo wataafikiana vizuri na wazalishaji wa umeme wa gesi.
“Ni vigumu kusema zitashuka kwa kiasi gani, lakini haziwezi kupanda,” alisema.
Mramba akiwa ameongozana na Meneja Miradi wa Tanesco, Injinia Simon Jilima, kuanza kuzalishwa kwa umeme wa gesi, tafsiri yake ni kwamba nchi haitakuwa na mgawo wa umeme, bei hazitapanda, lakini kuna uwezekano zikashuka kama gharama za uzalishaji hazitakuwa kubwa.
Alisema kukamilika kwa mtambo huo kumeenda sambamba na ujengaji wa mtandao wa vituo vya kupokea na kusambaza umeme, ambapo kwa Dar es Salaam vituo vinavyosambaza umeme wa hadi megawati 180 kwa wakati mmoja viko vine, Ubungo, Kipawa, Ilala City Center na IPTL.
Kuhusu vituo hivyo vinne na vingine vidogo, Injia Jilima alisema shirika limejenga mtandao wa kisasa wa kupokea na kusambaza umeme, ambapo kama eneo moja, mfano kituo cha Tandika kitapa hitilafu na kushindwa kusambaza umeme, wakazi wa eneo hilo wataendelea kupata umeme kutoka kituo kingine chochote, hata kilichopo Mikocheni.
Akizungumzia kupungua kwa gharama, Mramba alisema mtambo wa Kinyerezi utakapoanza wataachana na kampuni za Symbion na Aggreko, ambapo kwa kampuni ya IPTL wako kwenye mchakato wa kuanza kufua umeme kwa kutumia gesi.
Mramba alisema mtambo wa Kinyerezi utasaidia kuokoa Dola za Marekani milioni 70, ambazo Tanesco wamekuwa wakitumia kila mwezi kuzilipa kampuni hizo.
Kuhusu kuunganishia wateja wapya umeme, Mramba alisema wameanzisha program ya kuwaunganishia umeme wateja wa mijini ambapo kwa mujibu wa utafiti wao wa nchi nzima kwa maeneo ya mijini kuna wateja wapya 500,000.
Alisema program hiyo maalumun utatumia wakandarasi kuunganisha umeme kwa wateja na kwamba ndani ya miaka mitatu wateja hao watakuwa wameunganishiwa umeme, na kuanzia hapo Tanesco itakuwa na uwezo wa kuunganisha umeme kwa haraka kwa kila mteja anayeomba.

Zitto kumwachia cheo mgombea urais ACT

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema atalazimika kuachia wadhifa huo kwa mtu mwingine atakayeteuliwa na chama hicho kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho mwanachama anayeruhusiwa kugombea urais ni lazima awe kiongozi wa chama, wadhifa ambao unashikiliwa na Zitto ambaye hajafikisha umri wa kikatiba wa kugombea urais ambao ni kuanzia miaka 40. Kwa sasa ana miaka 39.
Zitto alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam juzi.
“Ikitokea hivyo (ACT ikapata mgombea urais, kutoka ndani au nje ya chama hicho), mimi natoka namwachia mtu mwingine na tumeshaamua hivyo, kwetu sisi tatizo siyo cheo. Tukipata mgombea urais leo nitampisha, sitakuwa kiongozi wa chama nitabaki kuwa mwanachama wa kawaida na mjumbe wa Kamati Kuu.”
Hata hivyo, alisema ili mtu huyo apate nafasi hiyo ni lazima aelewe malengo ya chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana.
“Tunataka mtu ambaye hata tukipata mabadiliko asiwe kikwazo cha hayo mabadiliko. Nasema hivi kwa sababu mnaweza kupata mtu mwingine kuwa kiongozi wa chama lakini baadaye anang’ang’ania na hataki kutoka,” alisema.
Alifafanua kuwa yeye bado ni kijana ana muda mrefu katika siasa na anaungwa mkono sehemu nyingi, hivyo hana haja ya kuharakisha katika kila jambo.
Hata hivyo, akizungumzia watu wa vyama vingine watakaojiunga na chama hicho alisema, “Kati ya watu watakaojiunga ACT au walioonyesha nia kutoka CCM au Ukawa hadi sasa hakuna ambaye ni mgombea urais.”
Alifafanua, “Sisi (ACT) tutasimamisha mgombea wetu wenyewe katika nafasi ya urais au tunaweza kumuunga mkono mgombea wa upinzani.”
Alisema watafanya hivyo kwa sababu hawataki kuua matumaini ya nchi kupata Serikali inayotokana na vyama vya upinzani, “Pale ambapo tutaona ni lazima kuunga mkono wenzetu kuing’oa CCM madarakani tutafanya hivyo. Si kama tunajiunga Ukawa, hapana ni kwa sababu bado hatujawa na mazungumzo nao na kujua nini kitakachotuunganisha.”
Sera na Ilani
Zitto aliziponda sera na ilani za vyama vya siasa nchini kwamba hazina tofauti, zote zina mfumo wa kiitikadi na mwelekeo uleule, isipokuwa kwa ACT Wazalendo.
Alisema kwa uzoefu wake wa miaka 10 akiwa mbunge na miaka saba akiwa mwenyekiti wa kamati za Bunge zinazoshughulikia matumizi ya Serikali,  amebaini kuwa nchi haiwezi kusonga mbele bila kubomoa mfumo uliopo.
“Ndiyo maana wakati wa uchaguzi vyama vinasema vitahakikisha vinapunguza matumizi ya Serikali kwa kupunguza malipo ya viongozi wa Serikali, lakini wakiingia bungeni hilo halitekelezwi kwa sababu kila mtu anafaidika na fedha hizo, hawezi kuubomoa mfumo,” alisema.
Alilifananisha suala hilo na posho za wabunge, matumizi ya magari ya kifahari ya Serikali lakini akisema kuwa hayo ni matumizi madogo ya Serikali kati ya mengi inayoyafanya.
Alisema ACT wanaanza kupambana na suala la matumizi ya viongozi mapema, ndio sababu ya kuweka kipengele katika katiba yao kinachowabana viongozi wa chama hicho kutangaza mali zao.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipendekeza uwepo wa miiko ya uongozi na kuiweka katika Rasimu ya Katiba, lakini hakuna chama cha siasa kilichoiweka miiko hiyo katika katiba yake.
“ACT tumeiweka miiko ya uongozi katika Katiba yetu. Tunajua kuwa tutapata wanasiasa wapya vijana na tunataka wajikute wakiwa katika mfumo huo kabla hata ya kuingia madarakani,” alisema.
Mwanasiasa huyo aliyelazimika kung’atuka ubunge baada ya kufukuzwa uanachama na Chadema, alisema kuna wabunge wanachanganyikiwa na fedha wanazopata mara baada ya kupata ubunge kutokana na kukua katika siasa bila kupitia katika vyama vinavyoheshimu miiko ya uongozi.
 “Mtu anakuwa mbunge mara baada ya kutoka chuoni, mshahara analipwa Sh11 milioni, mkopo wa gari Sh90 milioni na benki zinatoa mikopo ya Sh200 milioni. Wabunge wanachanganyikiwa.”
Akizungumzia kazi zinazofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana za kufanya ziara mikoani na kuisema Serikali inayoongozwa na chama hicho, alisema, “Uamuzi wa wananchi kumchagua mbunge ni tofauti na uamuzi wanaochukua kumchagua rais. Unaweza ukawa na mgombea mzuri wa ubunge mzuri lakini asiwe mgombea urais mzuri.”
Alisema Kinana anajitahidi lakini anakabiliwa na kazi ngumu ya kurejesha imani ya wananchi kwa CCM kwa maelezo kuwa imeshapotea kwa kiasi kikubwa.
Alisema katibu mkuu huyo angeweza kuifanya kazi hiyo vizuri kama angeshika wadhifa huo miaka 10 iliyopita.
“Kinana anapata watu wengi kwenye mikutano yake, anaongeza mambo mazuri lakini amekuwa mlalamikaji tu. Hatuoni malalamiko yake anayoyatoa kama yanafanyiwa kazi na Serikali yake,” alisema.Alisema kuwa katika Kamati Kuu ya CCM, Rais Kikwete ndio mwenyekiti wa kikao, hivyo Kinana anayeandika miniti hawezi kumfanya jambo lolote.

Contact Us

Phone :

+20 010 2517 8918

Address :

3rd Avenue, Upper East Side,
San Francisco

Email :

email_support@youradress.com