LIVERPOOL YAPIGA BEI MASTRAIKA WOTE
Gazeti la Daily Mail linafichua kwamba Liverpool imejiandaa kuwauza mastraika wake Mario Balotelli, Fabio Borini na Rickie Lambert mwishoni mwa msimu huu ili kupata pesa za kusajili nyota wa maana.
Straika Mtaliano, Balotelli amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Anfield kwa karibu msimu mzima baada ya kushindwa kufuatia uhamisho wake wa Pauni 16 milioni kutoka AC Milan mwaka jana.
Borini ameshindwa kupata namba kwenye kikosi hicho cha Brendan Rodgers, wakati Lambert anatumika mara chache sana kitu ambacho klabu hiyo inadhani anaongeza wingi tu kwenye kikosi chao.
Mastraika hao wote watatu wamecheza mechi 16 za Ligi Kuu England msimu huu na kwamba wataondoshwa Anfield wakati
dirisha la usajili wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa.
0 comments:
Post a Comment