KATIKA hali ya kushangaza, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alizua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella ‘King of The Best Melodies’
Mfano wa bastola ya Rey. “Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine aliyekuwa eneo hilo. Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila kupokelewa.