BASTOLA YA RAY YAZUA HOFU UKUMBINI
Mwandishi Wetu
KATIKA hali ya kushangaza, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alizua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella ‘King of The Best Melodies’
Muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’. Mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya
matukio ukumbini humo, aliwashuhudia watu waliomzunguka Ray wakionesha
hofu yao pale fulana yake ilipopanda juu na kuiacha bastola yake
aliyoichomeka kwenye suruali ikionekana bila kificho ambapo zaidi
walihofia mazingira ya unywaji wa pombe uliokuwepo. KATIKA hali ya kushangaza, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alizua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella ‘King of The Best Melodies’
“Jamani hii si hatari na ‘masanga’
haya anayogonga hapa ukimkorofisha hata kidogo tu si anaweza kukushuti
bila kuwaza nini kitatokea?,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa wamekaa
jirani na msanii huyo.Baadhi ya watu hao waliokuwa jirani na Ray
aliyekuwa amekaa pamoja na msanii mweziye Jacob Steven ‘JB’, walionekana
wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Mfano wa bastola ya Rey. “Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine aliyekuwa eneo hilo. Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila kupokelewa.

0 comments:
Post a Comment