Mamia ya wananchi wa kilosa na kilombero washiriki katika mazishi ya pamoja kwa abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Nganga.
Mamia ya wakazi wa wilaya za kilosa na kilombero wamejitokeza katika mazisha ya pamoja ya watu kumi na tano kati ya kumi na tisa waliofariki katika ajali ya basi ya nganga ambalo liligongana na fuso kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa mkoani Morogoro.
Wakizungumza kwa niaba ya serikali mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari amkoani wa Morogoro ili kudhibiti ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na vilemalema vya maisha ambapo mkuu wa wilaya ya kilombero Bw Lephy Gembe amewataka wananchi kuwa na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi wa wilaya hizo huku ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo siwakusahaulika kwani umewastua sana ambapo naye muinjilisti wa kanisa la kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na madereva wabovu.
0 comments:
Post a Comment