Kwa mara ya tatu mfululizo tangu 2012 shindano la kumsaka MR & Miss
Talent Mwenge Catholic University lilifana sana usiku wa kuamkia
jumamosi katika viwanja vya Kili Home Bar & Restaurant mkoani
Kilimanjaro na kufanikiwa kuwapata wale wanaolishikilia taji hilo hadi
pale mwaka 2016.
Shindano hilo ambalo lilijumuisha wadau mbali mbali toka viunga vyote
vya kanda ya kaskazini lilikuwa chini ya udhamini wa Serengeti breweries
kwa hisani ya kinywaji cha SMIRNOFF,Akiba Comercial Bank,Mwenge
Catholic University,Innosykes Computers,Image Transfers, Msafiri Maua
Medics pamoja na Kili Home Bar & Restaurant lilianza kupata uhai
majira saa mbili usiku hadi pale washindi walipopatikana.
 |
Washiriki wa kike waMr & Miss Talent Mwenge Catholic University wakicheza mbele ya waliohudhuria |
|
 |
Washiriki wa kiume waMr & Miss Talent Mwenge Catholic University wakicheza mbele ya waliohudhuria |
Katika kuhakikisha MR & Miss Talent anakuwa na vigezo vyote,
washiriki wapatao kumi na moja ambao ni wanafunzi wa Mwenge Catholic
University wakiwemo wasichana wanne na wavulana sita walitakiwa kuonesha
mitindo mbali mbali ya mavazi ikiwemo vazi la kawaida (casual wear)
,vazi la ofisini, vazi la usiku, ubunifu pamoja na vipaji vyao.
 |
Majaji wakiwa makini kutizama nini washiriki wanafanya |
Chini ya usimamizi mzuri wa Chief jaji Lui Ndakideme akisaidiana na
majaji Furaha Hamadi, Uenice Mmari pamoja na Mr Benson washiriki
walipata mchujo wa awali na kwa wale alioingia tano bora walikuwa ni
Samuel Sixbert,Mkude Robert,Raphael Nyandi Suzan Modest,Happy Munuo
pamoja na Noela Bernard Masao ambapo waliulizwa maswali na majaji na
baada ya hapo MR & Miss Talent wakatangazwa ambao ni Mkude Robert
Mwisaria na Noela Bernard Masao.
 |
Wawakilishi wa Akiba Comercial Bank nao walikuwa makini kufuatila kila tukio |
 |
Chief jaji Lui Ndakideme Kama
ilivyoada burudani ni sehemu muhimu ya shughuli kama hizi wasanii kadha
wakadha toka mkoani Kilimanjaro walipanda kwa steji na kuwatumbuiza
mamia ya wadau waliohudhuria kivutio kikubwa kikiwa ni "Diamond wa
Moshi" ambaye alokonga nyoyo za waliohudhuria halfa hiyo.
 |
Diamond wa Moshi akifanya yake stejini |
|
 |
Burudani ya sarakasi nayo ilikuwa sehemu ya tukio | FROM FUNGUKA LIVE | | | | | | | | | | | | | | |
0 comments:
Post a Comment