DJ VIRUS KUTOKA MOSHI ASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA DJ BORA UKANDA WA KASKAZINI YALIYOFANYIKA ARUSHA

DJ VIRUS AKIWA KATIKA AWAMU YA KWANZA YA MCHUANO
Ikiwa ni kwa
mara ya kwanza kampuni ya Viceroy kuandaa mashindano ya kumtafuta dj bomba
mwenye ujuzi mkubwa kwa ukanda wa kaskazini hatimaye mshindi apatikana.
Mashindano
haya yalifanyika jana jijini Arusha maeneo ya Club D ambapo judge mkuu wa
mashindano hayo alikuwa ni dj PQ kutoka clouds fm,clouds radio zilizopo jijini
Dar es Salaam.
Mashindano
haya ambayo yalisimamiwa na kampuni ya vinywaji vikali TDL(Tanzania Distillers
Limited) kupitia kinywaji chake cha Viceroy ambapo kupitia promotion zao waliweza
kutangaza mashindano hayo kupitia mikoa mitatu Manyara,Arusha pamoja na
Kilimanjaro.
Baada ya
kutoa fursa hiyo vijana wengi katika mikoa hiyo mitatu waliweza kuchukuwa fomu
zao za usaili kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ambayo fainali zake zilifanyikia
katika jiji la Arusha ndani ya club ya kisasa Afrika Mashariki iitwayo Club D.
Mpaka mwisho
wa tarehe ya kuchukua fomu tayari washiriki 15 waliweza kupatikana na hatimaye
kampuni hiyo iliweza kuandaa mchujo wa kwanza ambao waliweza kuwapata washiriki
8,siku iliyofuata mchujo mwingine uliweza kufanyika ambapo walipatikana ma Dj
watano bomba Dj Virus(Moshi), Dj Kito(Moshi), Dj Bray(Arusha), Dj Q(Arusha),
pamoja na Dj Ally(Arusha).
“Kiukweli
nimefurahishwa sana na mchuano huu lakini nimeweza kuona changamoto nyingi sana
kutoka kwa washiriki wetu moja ya changamoto ni mashine
ambayo walikuwa wanatumia washiriki, hii mashine ni kubwa sana(Pionner CDJ 800) hivyo ilikuwa ngumu sana kwa baadhi ya washiriki kuitumia”alisema Mr Mrema ambaye ni zone Manager wa kampuni hiyo.
ambayo walikuwa wanatumia washiriki, hii mashine ni kubwa sana(Pionner CDJ 800) hivyo ilikuwa ngumu sana kwa baadhi ya washiriki kuitumia”alisema Mr Mrema ambaye ni zone Manager wa kampuni hiyo.
Kabla ya
fainal hizo kufanyika washiriki wote watano waliweza kupata nafasi ya
kutembelea kituo cha redio kilichopo jijini Arusha kijulikanacho kama Radio 5
kuzungumzia juu ya fainali hizo ambapo kila dj aliweza kuzungumza kwa mtazamo
wake mwishoni wa mazungumzo kila dj aliweza kupewa nafasi ya kuonyesha ujuzi
wake katika mashine.
Hatimaye
siku ya jumamos fainali hizi ziliweza kufanyia pale club D Arusha ambapo
mchuano ulianza,Mzunguko wa kwanza ilianza kwa kila dj kupewa dakika tano za
kuonyesha ujuzi wake mpaka mwisho
waliweza kupatikana ma dj wanne Dj Virus(Moshi), Dj Kito(Moshi), Dj
Bray(Arusha), pamoja na Dj Ally(Arusha).
Baaa ya
kuwapata ma dj hao mzunguko wa pili ulianza kwa kila dj kupewa dakika 3 za
kuonyesha ujuzi wake tena na hatimaye hapo ndipo mshindi alipoweza kupatikana,
mshindi wa kwanza alitokea jijini Arusha Dj Bray, mshindi wa pili alitokea
Moshi Dj Virus na mshindi wa tatu alitokea Arusha, ushindi ambao ulitangazwa na
Dj PQ.
Mshindi wa
kwanza Dj Bray aliweza kuzawadiwa mashine aina ya Pionner CDJ 900 yenye thamani
ya shillingi million 8, mshindi wa pili Dj Virus alipewa headphone aina ya
beats by dre yenye thamani ya shillingi laki 4, saa,t-shirt-chupa ya Viceroy ya
ml 750 pamoja na kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomea u dj katika
chuo cha Dj PQ kwa muda wa miez mitatu bure na mshindi wa tatu Dj Ally aliweza
kupewa saa,t-shirt na chupa ya Viceroy ya ml 750.
Dhumuni hasa
la mashindano haya ni kuwafanya wale ma dj wote chipukizi waliopo katika
tathnia hii ya burudani ya muziki kuweza kuonekana na jamii kuwa wao pia
wanauwezo pamoja na kuwafanya waweze kupata ajira sehem tofauti tofauti.
DJ VIRUS AKIWA RADIO 5 ARUSHA AKIONYESHA UWEZO WAKE WAKATI WA MAHOJIANO
DJ VIRUS AKIWA CLUB D KWA NJE KABLA YA MASHINDANDO
CLUB D
DJ VIRUS AKIWA NA DJ PQ KUTOKA DAR ES SALAAM
BAADHI YA WASHIRIKI
0 comments:
Post a Comment