Arsenal, Man City kikaangoni
Manchester, England. England inaweza kukosa mwakilishi kwa mara
ya pili ndani ya miaka mitatu katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya kama Arsenal na Manchester City watashindwa kulipa kisasi
katika michezo yao ya leo na kesho.
Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 3-1 nyumbani
dhidi ya Monaco na sasa inakutana na miamba hiyo nchini Ufaransa, wakati
City ikitakiwa kugeuza kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Barcelona ili
kutinga katika robo fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Ni kazi ngumu kwa miamba hiyo ya England, lakini
inaweza kuchukua ari ya Schalke na Paris Saint-Germain waliopambana
ugenini wiki iliyopita.
Mabingwa watetezi, Real Madrid waliichapa Schalke
2-0 nchini Ujerumani, lakini hali ilikuwa mbaya nyumbani kwani waliitoa
timu hiyo kwa mabao 5-4, wakati PSG wakicheza 10 uwanjani dhidi ya
Chelsea tangu dakika ya 31, lakini walilazimisha sare na kusonga mbele
kwa mabao ya ugenini walipopata matokeo ya 2-2 Stamford Bridge.
Mechi nyingine wiki hii zinaonekana kuwa katika
uzani sawa. Bayer Leverkusen wataivaa Atletico wakiwa wameifunga Madrid
1-0 nchini Ujerumani na Juventus wataulinda ushindi wao wa 2-1 dhidi ya
Borussia Dortmund.
Arsenal wanaonekana
kuwa na mabadiliko wanapojiandaa kuivaa Monaco kutokana na kufanya vizuri katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu England.
kuwa na mabadiliko wanapojiandaa kuivaa Monaco kutokana na kufanya vizuri katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu England.
Ushindi dhidi ya Everton, QPR na West Ham katika
ligi na ule dhidi ya Manchester United katika Kombe la FAumeufanya msimu
wa Arsenal kuwa mzuri na wanatakiwa kuwa na kasi hiyo katika Uwanja wa
Louis II.
Safu ya ulinzi ya Monaco imeonekana kuwa ngumu
msimu huu ikiwa imeruhusu mabao 20 katika michezo 28 ya Ligi Kuu
Ufaransa, lakini pia wameonyesha ukomavu kwa kufungwa na PSG na Bordeaux
pekee.
Lakini pia, Arsenal haijawahi kupoteza mchezo
nchini Ufaransa ikiwa na rekodi nzuri na timu za nchi hiyo katika
michezo ya marudiano.
Hata hivyo, Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim
amekuwa na matumizi mazuri ya mashambulizi ya kushitukiza yaliyomsaidia
katika mchezo wa kwanza dhidi ya Arsenal.
Licha ya Lionel Messi kukosa penalti katika mchezo
wa kwanza, Man City wanatakiwa kuwa makini na kikosi hicho watakapokuwa
katika Uwanja wa Camp Nou kesho.
Leo, Jumanne
A.Madrid v B.Leverkusen (Saa 4:45 usiku)
Monaco v Arsenal (Saa 4:45 usiku)
Kesho, Jumatano
B.Dortmund v Juventus (Saa 4:45 usiku)
Barcelona v Man City (Saa 4:45 usiku)
LIGI YA MABINGWA ULAYA
0 comments:
Post a Comment