WAKULIMA NCHINI WANATARAJIA KUNUFAIKA NA MRADI MPYA WA KILIMO CHA NDIZI NA VIAZI VITAMU
Mradi huo
wa miaka minne uliopewa jina la 'Mbegu, Mkulima, Soko na Mlaji
(SeFaMaCo)' una lengo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo la usalama wa
chakula na kupambana na umaskini katika nchi za Tanzania, Uganda na
Ethiopia.
Mradi huo unafadhiliwa na Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF), na kutelelezwa na taasisi ya Farm Concern International (FCI).
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mradi huo mwishoni mwa wiki, Meneja wa Programu ya SeFaMaCo, Winston Mwombeki, alisema mradi huo unalenga kukuza uzalishaji wa mazao hayo katika nchi husika.
Alisema kwa upande wa Tanzania, mradi huo utanufaisha kaya zipatazo 94,000.
Alisema mikoa ambayo imelengwa kwa uzalishaji wa viazi ni Kagera, Mwanza, Morogoro na Zanzibar, wakati Uganda, mradi huo utafanyika katika mikoa ya Kamuli/Buyende, Soroti, Gulu na Lira.

Kwa upande wa Ethiopia, mradi huo utatekelezwa katika mikoa ya Wolaita, Sidama na Gamogofa.
Kwa upande wa kilimo cha ndizi, mikoa ambayo imelengwa nchini ni Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar, Morogoro wakati kwa upande wa Uganda ni Mbarara/Isingiro, Masaka (Bukomansimbi na Lwengo) na Kabale.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Twahir Nzallawahe, waliwataka wakulima katika maeneo husika ya mradi, kujikita katika mradi huo kutokana na manufaa yake.
"Tumebuni ushirikiano ambao utatafsiri kuwaingiza mamia kwa maelfu ya wakulima kama mnyororo wa wadau muhimu wa kilimo cha ndizi na viazi na kuongeza mnyororo wa thamani ya chakula," alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alipongeza kuanzishwa kwa mradi huo, akisema utaliongezea taifa thamani mpya katika uzalishaji wa chakula nchini.
Aliwataka wakulima wadogo wadogo nchini kujikita katika uzalishaji wa ndizi na viazi kwa sababu mazao hayo yanavirutubisho vingi na yanaweza kuongeza uchumi.
Kiongozi wa Programu ya SewFaMaCo, Stanley Mwangi, alisema mradi huo unatarajiwa kanufaisha kaya 192,000 katika nchi za Afrika.
Alisema ndizi na viazi zinatoa fursa kwa wakulima wengi kuhusu umuhimu wa kufanya utafiti.
from mjengwa blog
0 comments:
Post a Comment